Wednesday, August 8, 2012

CHADEMA Kufanya mkutano mkubwa wa operation sangara leo ifakara


Baada ya zengwe walilowekewa na polisi pale morogoro,na kuwazuiwa kufanya mikutano ya hadhara, leo chadema watafanya mkutano wa kufa mtu hapa mjini ifakara. Kwa mujibu wa radio pambazuko na vipeperushi, operation sangara maalum ya kukipanga chama tayari kukabidhiwa dola inazinduliwa leo 8/8/2012. Viongozi wote wa kitaifa ,kamanda Freeman Mbowe, mpiganaji Dr Wilbrod Slaa,makamu mwenyekiti Said Afri,mbunge wa kigoma kaskazini Zitto kabwe, J.J Mnyika na mwanasheria Mabere Marando wote watakuwepo. Pia wabunge wote wa cdm watakuwepo. Mkutano utafanyika viwanja vya polisi maarufu kama kiungani. Mapokezi ni pale kibaoni saa 7:00 mchana, yakifatiwa na maandamano kuelekea viwanjani. Mkutano utaanza saa 8:30. ITV, STAR TV na Chanel ten watakuwepo. Ntakuwa up 2 date. Kwa sasa ni mzuka pikipiki zinapita mitaani zikipeperusha bendera za cdm.

No comments:

Post a Comment